Main Title

source : Parstoday
Jumanne

12 Machi 2024

19:45:32
1443997

UNFPA: Wanawake ni waathirika wakubwa wa mfumo wa afya usiofanya kazi wa Yemen

Naibu Mwakilishi wa Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) nchini Yemen ameeleza kuwa aghalabu ya hospitali na vituo vya afya nchini humo havifanyi kazi kutokana na hali ya mgogoro iliyoikumba nchi hiyo na hivyo kusababisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.

Nchini Yemen, chini ya asilimia 50 ya hospitali na vituo vya afya ndivyo vinavyofanya kazi; na  moja  ya tano tu ya vituo hivyo vya afya vinatoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga.Naibu Mwakilishi wa Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) huko Yemen, Hicham Nahro ameongeza kuwa, wanawake wajawazito wanashindwa kufika mahospitalini na kwenye vituo vya afya vinavyotoa huduma kwa wajawazito kutokana kuhama mara kwa mara na kuishi vijijini na katika maeneo ya mbali. Hicham Nahro amesema familia zinazoishi vijijini pia hazina uwezo wa kwenda hospitali au katika vituo vya afya kutokana na kukosa fedha. "Familia nyingi za Wayemeni haziwezi kumudu gharama za hospitali na hata gharama za usafiri kufika kwenye vituo vya afya mijini", amesema. Naibu Mwakilishi wa UNFPA nchini Yemen amesema mfuko huo mwaka jana uliweza kuwafikia wanawake na wasichana karibu milioni tatu wa Yemen, hata hivyo bado kuna haja kubwa ya kutolewa misaada ili kusaidia mchakato wa afya ya mama mjamzito nchini humo. Mgogoro wa sasa wa Yemen ni matokeo ya vita vya pande zote vilivyoanzisha mwaka 2015 na muungano vamizi chini ya uongozi wa Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo .   

342/