Main Title

source : Parstoday
Jumanne

12 Machi 2024

19:46:50
1443999

Rabi mkuu wa Wayahudi atishia kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu

Rabi Mkuu wa Wayahudi, Ishaq Yosef, ametishia kuwa wataondoka wote Israel iwapo kabila la Lawi litalazimishwa kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni.

Kuhani Ishaq Yosef ameeleza kuwa watu wa kabila la Lawi hawalazimiki kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba jambo hili halipasi kutekelezwa kwa hali yoyote ile. 

Wakati huo huo Benny Gantz, waziri katika baraza la mawaziri la vita la Israel ameitaja hatua ya Ishaq Yosef, Rabi Mkuu wa Wayahudi ya kutishia kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) na sisitizo lake la kutojiunga na jeshi kabila la Lawi kuwa ni maafa ya kimaadili kwa jamii ya Israel na kusema: Watu wote, hata Mayahudi wenye msimamo mikali, wanapasa kuhudumu jeshini katika kipindi hiki kigumu.  Kauli hiyo ya Rabi Mkuu wa Israel imeibua mshtuko mkubwa huko Israel. 

342/