Main Title

source : Parstoday
Jumanne

12 Machi 2024

19:47:22
1444000

Makamu wa Rais wa Iran ataka utawala wa Kizayuni utimuliwe kwenye kamisheni ya wanawake ya UN

Ensiyeh Khazali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke kuwa, utawala wa Kizayuni lazima utimuliwe kwenye kamisheni hiyo kutokana na jinai zake za miongo kadhaa za kuua mamilioni ya wanawake na watoto wadogo.

Press TV na Shirika la habari la IRNA leo Jumanne limemnkuu Bi Ensiyeh Khazali akisema hayo kwenye Kikao cha 68 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai dhidi ya mamilioni ya wanawake na watoto wadogo kwa miongo kadhaa sasa, hivyo haina nafasi kwenye kamisheni hiyo. 

Ameongeza kuwa mamilioni ya wanawake na watoto wa Palestina wanaishi kwenye mazingira magumu ya ukimbizi kwa miongo mingi kutokana na uvamizi na jinai za Israel.

Amesema: "Natumia fursa hii, kuwakilisha wanawake imara wa Iran na kuungana na wanawake wenye heshima wanaopigania amani na usalama duniani kupaza sauti na kutaka kufutwa uanachama wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye kamisheni hii."Makamu huyo wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kutimuliwa Israel kwenye Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke katika hali ambayo, kutokana na uungaji mkono wa pande zote wa madola ya kibeberu ya Magharibi hasa Marekani, Uingereza na Ujerumani, utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai za kutisha dhidi ya wanawake na watoto wadogo huko Ghaza, Palestina. Utawala huo dhalimu unafanya juhudi zilizoshindwa za kujaribu kufifiliza kipigo ulichokipata kutokana na operesheni ya kishujaa ya Wapalestina ya Kimbunga cha al Aqsa. Ripoti zinasema kuwa, wakati vita angamizi vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza vikiwa vimeingia mwezi wa sita sasa, zaidi ya Wapalestina 31,450 wameshauawa shahidi na zaidi ya 72,654 wameshajeruhiwa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.

342/