Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:40:44
1444245

Intelijensia ya Marekani: HAMAS itaendelea kutoa changamoto kwa Israel kwa "miaka kadhaa"

Ripoti ya tathmini ya kiintelijensia iliyotolewa na Marekani imetilia shaka uwezo wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuifuta Hamas, harakati hiyo ya muqawama ya Palestina huenda ikatoa changamoto "ya muda mrefu" kwa miaka kadhaa kwa utawala huo ghasibu unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.

Ripoti ya "Tathmini ya Tishio ya Mwaka 2024", ambayo ilitolewa siku ya Jumatatu, imetabiri kwamba Israel "itapambana sana" kufikia lengo lake lililotangazwa la "kuiangamiza Hamas" katika vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Ripoti hiyo imesema: Israel yamkini itakabiliwa na mapambano ya mtutu wa bunudki ya Hamas kwa miaka kadhaa ijayo, na jeshi la utawala huo litapambana sana kuweza kudhoofisha miundombinu ya chini ya ardhi ya Hamas. Tathmini hiyo aidha imetahadharisha kuwa hatari ya kupanuka vita vya Ghaza, ambavyo sasa viko katika mwezi wake wa sita, "ingali iko juu." Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mashambulizi dhidi ya Ghaza "yanatoa changamoto" kwa washirika Waarabu wa Marekani kutokana na kuongezeka kwa hisia za chuki za umma wa Waarabu dhidi ya Israel na Marekani zinazosababishwa na "vifo na uharibifu unaofanywa huko Ghaza. Ripoti hiyo ya kiintelijensia ya Washington imetabri pia kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel utazidi kukabiliwa na mashinikizo ya kimataifa kwa sababu ya hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza.Sehemu nyingine ya ripoti hiyo imetabiri pia kuwa,  Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon itaendeleza mashambulizi yake katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel katika muda wote wa vita vya Ghaza.Kulingana na tathmini hiyo ya kiintelijensia, operesheni za Hizbullah zinalenga "kuwabana wanajeshi wa Israel" wakati wanajaribu kuiangamiza Hamas huko Ghaza".Aidha, ripoti hiyo imeeleza bayana kuwa Iran "haikupanga wala haikuwa na taarifa kabla" kuhusu operesheni ya Hamas ya tarehe 7 Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.../