Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:41:14
1444246

Waisraeli 80,000 wakimbia makazi yao wakihofia makombora ya Hizbullah

Makumi ya maelfu ya walowezi wa Kizayuni wamekimbia makazi yao katika maeneo ya kaskazini mwa Palestina yaliyopachikwa jinai bandia la Israel, wakihofia mashambulizi ya Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Jenerali Tamir Hayman, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya jeshi la utawala haramu wa Israel amesema walowezi 80,000 wa Kiyahudi wamelazika kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya kaskazini, baada ya kutiwa wahaka na hujuma za makombora ya Hizbullah.

Jenerali Hayman amekiri kuwa, kuendelea kwa mashambulizi ya Hizbullah katika maeneo hayo ya kistratajia yaliyoko mpakani na Lebanon ni kwa maslahi ya mrengo wa mapambano ya Kiislamu. 

Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon kwa miezi kadhaa sasa umeendelea kupiga kwa makombora kambi za kijeshi na maeneo mengine ya Kizayuni huko kaskazini mwa Palestina yaliyopachikwa jinai bandia la Israel.

Hizbullah ya Lebanon imesisitiza kuwa, harakati hiyo ya muqawama inafanya mashambulizi yake dhidi ya Wazayuni kujibu mashambulio ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kwamba uungaji mkono wa kivitendo wa Hizbullah kwa wakazi wa Gaza utaendelea.Mapema jana Jumanne, muqawama wa Lebanon ulikipiga kwa makombora zaidi ya 100 ya Katyusha, kituo kikuu cha ulinzi wa anga cha utawala wa Kizayuni katika maeneo ya kaskazini mwa Palestina yaliyopachikwa jinai bandia la Israel. Viongozi wa Hizbullah wanasema kuwa, madhali uvamizi wa Israel huko Gaza unaendelea, harakati hiyo ya mapmabano ya Kiislamu nayo itaendelea kuushambulia utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono kivitendo watu wa Gaza.