Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:41:35
1444247

Mamia ya walowezi wa Kiyahudi wauvamia Msikiti wa Al-Aqsa huku wakilindwa na askari wa Israel

Mamia ya walowezi wa Kiyahudi jana Jumanne walivamia tena eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Baitul-Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu huku wakisindikizwa na kulindwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanaoendelea kuchukua hatua kali za kuwawekea mipaka Wapalestina ya kuingia kwenye msikiti huo.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Palestina Wafa, walowezi hao wa Kizayuni walivamia Msikiti wa Al-Aqsa kwa makundi kutokea eneo la Babul-Mughaaribah upande wa magharibi wa msikiti huo mtakatifu. Mapema siku ya Jumatatu, walowezi wapatao 275 wa Kiyahudi waliingia kwenye eneo la jengo la Msikiti wa Al-Aqsa kwa wito uliotolewa na makundi ya Kiyahudi yenye chuki na itikadi kali wa kushadidisha hujuma na uvamizi katika msikiti huo wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

342/