Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:41:55
1444248

Amir-Abdollahian: Israel inatekeleza kwa makusudi sera za kuliangamiza taifa la Palestina

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, moja ya malengo hatari ya utawala ghasibu wa Israel katika kuizingira kikamilifu Gaza na kuzuia kutumwa misaada ni kuandaa mazingira ya kusambaratika kijamii na kiraia Ukanda huo.

Hussein Amir-Abdollahian ameeleza kuwa, Israel inatekeleza sera hizo ili kutokomeza dalili zote za maisha ya Wapalestina pamoja na utambulisho wao na kuwahamisha wakazi wa eneo hilo kwa nguvu.

Abdollahian amesisitiza kuwa, hii inathibitisha kwamba utawala dhalimu wa Kizayuni unatekeleza kwa makusudi siasa za kuliangamiza kabisa "taifa la Palestina na utambulisho wake."

Abdollahian amesema hayo katika barua aliyoituma kwa Makatibu Wakuu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi za Kiislamu ambapo amesema kuhusu matukio ya Palestina kwambna,: Katika hali ambayo inashuhudia kuendelea kutokuwa na uwezo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kusitisha vita dhidi ya Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na Marekani kukwamisha kwa makusudi juhudi za kufikia hilo,  kuna haja kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dhati za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina, kusimamishwa vita haraka na kuliondoa eneo hilo katika hali mbaya ya sasa inalokabiliwa nalo.