Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:43:06
1444251

Vladimir Putin: Russia iko tayari kwa vita vya nyuklia

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, nchi yake iko tayari kutumia silaha za nyuklia ikiwa kutakuwepo tishio kwa serikali na uhuru wake.

Kauli hiyo ya Rais Putin ni kama onyo la wazi dhidi ya mataifa ya Magharibi kabla ya uchaguzi mkuu wa rais wiki hii nchini Russia ambapo Putin ana kubwa ya kuibuka na ushindi na hivyo kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka sita.

Rais Putin ametoa ontyo hilo katika mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha televisheni cha serikali ya Russia yaliyorushwa hewani leo.  Putin alimuelezea Rais Joe Biden wa Marekani kama mwanasiasa mkongwe anaelewa kikamilifu hatari zinazoweza kutokea ikiwa mzozo utatanuka lakini akasema kuwa, hafikirii kuwa ulimwengu unaelekea kwenye vita vya nyuklia.

Wakati huo huo, rais Putin amesisitiza kuwa vikosi vyenye dhamana ya silaha za nyuklia vya Russia vimejitayarisha kikamilifu huku akisema kuwa mifumo ya silaha za nyuklia ya nchi hiyo iwe ya angani, majini na ardhini ni bora zaidi. 

Rais Putin amesema kama ninavyomnukuu: " Kwa mtazamo wa kijeshi na kiufundi, bila shaka, tuko tayari kwa vita vya nyuklia. Wanajeshi wa Russia daima wako katika hali ya utayari wa kupambana. Hili ndilo jambo la kwanza. Pili, kwa ujumla, mifumo yetu ya nyuklia ni ya kisasa zaidi kuliko mingine yoyote. Ni sisi tu na Marekani ambao tuna mifumo kama hii. Lakini mifumo yetu ni ya kisasa zaidi."

Aidha, rais huyo wa Russia ameendelea kusema kuwa, ikiwa washirika wa Ukraine watatuma wanajeshi kuisaidia nchi hiyo iliyokumbwa na vita, hilo halitobadili chochote katika uwanja wa vita kama ilivyokuwa kwa hatua yao ya kuipatia Ukraine silaha.

342/