Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:43:27
1444252

Wajumbe wa Baraza la Seneti wamtaka Biden aache kuipatia Israel msaada wa silaha

Wajumbe wa Baraza la Seneti la Marekani wamemuandikia barua Rias wa nchi hiyo Joe Biden wakimtaka aache kuipatia silaha Israel ambayo imekuwa ikifanya mauaji dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Duru za karibu na Seneti ya Marekani zinasema kuwa, wawakilishi 7 wa baraza hilo kutoka chama cha Kidemokrasia na Bernie Sanders mwakilishi wa kujitegemea wa jimbo la Vermont wamemuandikia barua Biden na kumtaka asitishe mara moja misaada ya kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wajumbe hao wamesema katika barua hiyo kwamba, Joe Biden anapaswa kumueleza wazi na bayana Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel kwamba, kutofika misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutakuwa na matokeo mabaya sana.

Pia wamesisitiza kwamba, hatua za Netanyahu zinakiuka kifungu cha himaya na uungaji mkono wa kibinadamu katika Sheria ya Misaada ya Kigeni ya Marekani.

342/