Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Machi 2024

20:43:55
1444253

Malaysia: Tunaunga mkono kwa dhati Muqawama wa Palestina dhidi ya uvamizi wa Israel

Waziri Mkuu wa Malaysia amesema anaunga mkono kwa dhati Muqawama wa makundi ya Wapalestina dhidi ya mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Anwar Ibrahim ametangaza msimamo huo baada ya mazungumzo yake na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani yaliyofanyika mjini Berlin, wakati akitetea uhusiano wa nchi yake na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na kusisitiza kuwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ulikuwa ni mwanzo wa hatua ya kukabiliana na miongo kadhaa ya "ukatili, uporaji na unyang'anyi wa milki" uliofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.Mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya Muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Ghaza na kushambulia ngome za utawala wa Kizayuni likiwa ni jibu kwa jinai za miongo saba za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina.

342/