Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

15 Machi 2024

13:56:12
1444569

Ansarullah: Operesheni za kushambulia meli zenye uhusiano na Israel zitapanuliwa hadi Bahari ya Hindi

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sayyid Abdul Malik Al-Houthi amesema askari wa jeshi la nchi hiyo wataendelea na operesheni zao za kujibu mapigo dhidi ya meli za kibiashara zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kuzizuia meli hizo kupita hata kwenye eneo la maji ya Bahari ya Hindi na Rasi ya Tumaini Jema.

Katika hotuba aliyotoa usiku wa kuamkia leo, Abdul Malik Al-Houthi amebainisha kuwa, apiganaji wapatao 34 wa harakati ya Ansarullah wameuawa shahidi tangu wanajeshi wa Yemen walipoanza kushambulia misafara ya meli kuonyesha mshikamano na Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza wanaoandamwa na mashambulio ya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na jeshi katili la utawala wa Kizayuni. Kuanzia katikati ya mwezo Novemba 2023, vikosi vya Yemen vimerusha mara kadhaa ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya meli za utawala wa Kizayuni na zinazoelekea kwenye bandari za utawala huo tangu, vikisisitiza kuwa vinachukua hatua hiyo kuonyesha mshikamano na Wapalestina wanaokabiliwa na vita vya Israel dhidi ya Ghaza. Katika hotuba yake hiyo, Kiongozi wa Ansarullah amesema, hadi sasa meli 73 zimelengwa katika operesheni za Yemen za kuiunga mkono Ghaza, na akaongeza kuwa, ni nadra sasa kwa meli yoyote yenye uhusiano na na adui Mzayuni kupitia lango bahari la Bab al-Mandab.

Amefafanua kwa kusema: "wiki hii, operesheni za usaidizi zilijumuisha operesheni 12 zilizolenga meli na mashua, zilizotekelezwa kwa kutumia jumla ya makombora 58 ya balestiki na ya kruzi pamoja na droni katika Bahari Nyekundu, Bahari ya Arabia na Ghuba ya Aden".

 Sayyid Abdul Malik Al-Houthi ameendelea kueleza: "operesheni zetu mara hii zimefikia umbali ambao haujawahi kushuhudiwa, na kwa rehma za Mwenyezi Mungu operesheni tatu zilifika Bahari ya Hindi " na akaongezea kwa kusema: "idadi ya meli zote na mashua zilizolengwa hadi sasa imefikia 73". Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa operesheni hizo zitaendelea maadamu hujuma na mzingiro dhidi ya Ghaza unaendelea. Marekani na Uingereza zilianza kuishambulia Yemen mwezi Januari ili kuizuia nchi hiyo kuzilenga meli za Israel zinazobeba silaha na vifaa kwa ajili ya mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza uliozingirwa. Abdul Malik Al-Houthi amebainisha kuwa Wamarekani na Waingereza wamepata "mapigo machungu" kutokana na wanajeshi wa Yemen kujibu mapigo kwa hatua zao za kichokozi dhidi ya nchi hiyo.../


342/