Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

15 Machi 2024

13:58:20
1444573

Amir-Abdollahian: Adui Mzayuni hajaweza kufikia malengo yake katika vita vya Ghaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, adui Mzayuni hajaweza kufikia hata moja kati ya malengo aliyoyatangaza kuhusiana na vita vya Ghaza. Amir-Abdollahian ameyasema hayo katika salamu zake kwa viongozi wa makundi ya muqawama na wananchi wenye istikama na subira wa Lebanon na Palestina ambapo sambamba na kuenzi kumbukumbu za mashahidi wa Muqawama ametoa mkono wa kheri na baraka pia kwa mnasaba wa kuandama mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa IRNA, katika salamu zake hizo za pongezi kwa Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS na Ziad Al-Nakhlah, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: kwa kuandama mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa machipuo ya Qur'ani na mwezi wa kuhudhuria ugeni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ninakupeni mkono wa pongezi nyinyi na vikosi vyote vya muqawama na mujahidina wanaokabiliana na utawala wenye kuchukiza na mtenda jinai wa Kizayuni, na vile vile kwa familia zote tukufu za Mashahidi na majeruhi wa vita vya sasa, na pia kwa wananchi wenye istikama na subira wa Lebanon na Palestina.

Katika salamu zake hizo, Amir-Abdollahiana ameongeza kuwa: Waislamu duniani wameukaribisha mwezi huu mtukufu katika hali ambayo utawala unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu unaendelea kufanya jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hususan wanawake na watoto wanaodhulumiwa wa ardhi hii takatifu, na hakuna hatua za maana zilizochukuliwa na taasisi husika za kimataifa, likiwemo Baraza Usalama wa Umoja wa Mataifa za kukomesha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel.

 Aidha ameendelea kueleza kwamba: kwa upande mwingine, mkabala wa jinai kubwa zinazofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni na kutochukuliwa hatua zozote na watetezi bandia wa haki za binadamu, tunashuhudia muqawama wa kishujaa, wa kujivunia na wa kihistoria wa vikosi vya muqawama na wananchi wenye ghera wa Palestina katika kukabiliana na utawala huo uliojizatiti kwa silaha huku ukiungwa mkono kwa kila hali na serikali ya Marekani; na kutokana na jihadi na istikama ya heshima na izza, adui Mzayuni hajaweza kufikia hata moja kati ya malengo aliyoyatangaza na athari za pigo la kihistoria la kushindwa utawala huo zimejitokeza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kwa kusema, "kwa imani ya dhati ya moyoni na ya uumini wa kweli juu ya kuthibiti kiuhakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi, katika siku na mikesha hii yenye fadhila na utukufu, ninaienzi kumbukumbu ya Mashahidi wote wa Muqawama, na ninamwomba Mwenyezi Mungu alipe ushindi kamili taifa la Palestina na kukombolewa kwa Quds Tukufu.../


342/