Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

15 Machi 2024

13:59:00
1444574

Iran yalaani kupewa uanachama Israel kwenye Baraza la Haki za Binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni ambao unafanya mauaji ya kimbari dhidi ya watoto wadogo huko Palestina haustahiki kabisa kuwa mwanachama wa mashirika ya haki za binadamu na ya misaada duniani likiwemo baraza la kupigania haki za wanawake la Umoja wa Mataifa.

Naser Kan'ani amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X na huku akigusia jinai za kutisha zinazofanywa na Israel hivi sasa dhidi ya wanawake, watoto wadogo na raia wa kawaida huko Ghaza amesema kuwa, mashirika ya misaada ya kimataifa ambayo yenyewe hayajasalimika na jinai za utawala wa Kizayuni, hayapaswi kuupa uanachama utawala huko katili.

Kabla ya hapo pia, Bi Ensiyeh Khazali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema siku chache nyuma katika kikao cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke kwamba, utawala wa Kizayuni lazima utimuliwe kwenye kamisheni hiyo kutokana na jinai zake za miongo kadhaa za kuua mamilioni ya wanawake na watoto wadogo.Jumanne wiki hii, Press TV na Shirika la habari la IRNA lilimnkuu Bi Ensiyeh Khazali akisema hayo kwenye Kikao cha 68 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Nafasi ya Mwanamke na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai dhidi ya mamilioni ya wanawake na watoto wadogo kwa miongo kadhaa sasa, hivyo haina nafasi kwenye kamisheni hiyo. Aliongeza kuwa mamilioni ya wanawake na watoto wa Palestina wanaishi kwenye mazingira magumu ya ukimbizi kwa miongo mingi kutokana na uvamizi na jinai za Israel. Zaidi ya vituo 150 vya shirika la UNRWA la Umoja wa Mataifa zikiwemo skuli vimeshambuliwa na kuharibiwa kikamilifu na utawala wa Kizayuni katika vita vya hivi sasa vya Ghaza na zaidi ya Wapalestina 400 hivi sasa wamekosa maeneo ya kukimbilia kutokana na kuharibiwa vituo vya shirika hilo.