Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Machi 2024

19:29:06
1444898

Rais wa Marekani aunga mkono kutimuliwa uongozini Benjamn Netanyahu

Rais wa Marekani amempongeza kiongozi wa viti vingi katika Baraza la Sanate la nchi hiyo kutokana na mwito wake wa kutaka kutimuliwa madarakani Benjamin Netanyahu na kuitishwa uchaguzi wa kabla yake ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Joe Biden amelazimika kuchukua msimamo ulio dhidi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu na kuunga mkono kuitishwa uchaguzi wa kabla ya wakati wake huko Israel kutokana na kuzidi kulaumiwa serikali ya Marekani kutokana na uungaji mkono wake wa kupindukia kwa jinai za utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa televisheni ya BBC ambacho ni chombo cha habari cha utawala wa kifalme wa Uingereza, Biden hakutamka moja kwa moja kuwa anaunga mkono kutimuliwa madarakani Benjamin Netanyahu, lakini amempongeza mkuu wa viti vingi vya chama cha Democratic huko Marekani kwa mwito wake wa kutaka kuitishwa uchaguzi wa mapema ndani ya utawala wa Kizayuni.Kwa mujibu wa ripota wa BBC, matamshi hayo ya Biden aliyoyatoa wakati wa mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Ireland katika Ikulu ya Marekani, White House, huenda ni ishara ya kuongezeka mpasuko baina ya Tel Aviv na muitifaki wake wa karibu mno yaani Marekani. Maafisa wa serikali ya Benjamin Netanyahu wamelalamikia vikali matamshi ya kiongozi wa Wademocrat katika Baraza la Sanate la Marekani na kudai kuwa, siasa za waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni eti zinaungwa mkono na watu wengi. Madai hayo ya viongozi wa chama cha Netanyahu yametolewa katika hali ambayo maandamano makubwa ya kupinga serikali ya Benjamin Netanyahu inayoongozwa na Wazayuni wenye misimamo mikali, kukipinga chama cha Likud na Benjamin Netanyahu mwenyewe, yanaendelea kwa muda mrefu sasa ndani ya utawala wa Kizayuni.