Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Machi 2024

19:33:32
1444903

Jihadul Islami: US na Isreal zinafuatilia malengo sawa Gaza

Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema pamoja na unafiki na hadaa za Marekani, lakini dola hilo la kiistikbari linafuatilia malengo yanayoshabihiana na ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Mohammad al-Hindi, Naibu Katibu Mkuu wa harakati hiyo ya muqawama yenye makao yake huko Gaza amesema hayo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na kanali ya Press TV na kuongeza kuwa, lengo la Tel Aviv na Washington ni kuendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Al-Hindi amesema: Katika uvamizi huu, kuna mapatano baina ya Marekani na Israel. Utawala wa Marekani ni mshirika kamili wa Israel, licha ya (Marekani) kububujikwa na machozi ya mamba.

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Jihadul Islami ya Palestina ameongeza kwa kusema, malengo ya kistratajia ya Marekani na Israel katika vita dhidi ya Gaza ni kuusambaratisha muqawama, ijapokuwa vipaumbele vya Washington na Tel Aviv vinatofautiana.Amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni haujafikia malengo yake yoyote huko katika Ukanda wa Gaza, kutokana na wananchi wa Palestina kusimama kidete na wameweza kuusababishia hasara na pigo kubwa utawala wa Kizayuni. Kadhalika Mohammad al-Hindi, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islamu ya Palestina amesema Marekani inabeba dhima ya mauaji ya kimbari Gaza, na kwamba kitendo cha Washington kujifanya kinawadondoshea wakazi wa Gaza misaada ya chakula kutoka angani ni unafiki mwingine wa Washington.

342/*