Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Machi 2024

19:34:53
1444906

Kan'ani: Ndoto za kuigawa vipande vipande Iran zitazikwa kwenye kaburi la sahau

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu matamshi ya kijuba na ya kipuuza na kiongozi mmoja wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kuwa, ndoto za kuigawa vipandevipande Iran zitazikwa kwenye kaburi la sahau kama zilivyozikwa njozi nyingine za maadui.

Shirika la habari la Tasnimn limemnukuu Nasser Kan'ani akisema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X na kumjibu Mordechai Kedar, afisa wa zamani wa masuala ya usalama ya utawala wa Kizayuni akimwambia, ndoto zenu za kuigawa vipande vipande Iran mtazikwa nazo kaburini.

Mzayuni huyo ametoa matamshi ya kifidhuli kwa kudai kuwa eti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lazima igawanywe kwenye nchi 6 ndogondogo kwa mujibu wa kaumu na makabila yake.Kan'ani amejibu matamshi hayo ya kijuba na yaliyojaa chuki akisema: Mzayuni huyu ambaye hivi sasa amepooza na yuko juu ya kigari cha wagonjwa, hata mwaka jana pia alichochea kufanyika mashambulizi ya kijeshi ya Wazayuni dhidi ya nchi mbalimbali na kutamka wazi kuwa 'lazima tuigawe vipande vipande Iran' lakini hivi sasa yeye mwenyewe amepooza na anatembelea kigari cha wagonjwa na kuicha Jamhuri ya Kiislamuu ikiendelea kuwa imara. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, ingawa hii si mara ya kwanza kwa adui Mzayuni kutoa matamshi ya kifidhuli na kijuba kama hayo, lakini kwa mara nyigine tunapenda kuwaambia Wazayuni na maadui wote kwamba hivi sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imo kwenye muongo wake wa nne na kila siku inazidi kustawi, hivyo haitetereshwi na matamshi ya chuki kama ya Mzayuni huyu. Ameongeza kuwa, kwa zaidi ya miongo minne sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakabiliana kiume na njama za kila namna za adui na katika siku za usoni pia itaendelea hivyo hivyo na itazidi kuwakatisha tamaa maadui.

342/