Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Machi 2024

19:37:00
1444908

Marekani ndiye mshutumiwa nambari moja wa kuvunja haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani ndiye mshutumiwa nambari moja wa uvunjaji wa haki za binadamu hasa hivi sasa ambao unausheheneza silaha za mauaji ya kimbari utawala wa Kizayuni wa Israel.

Nasser Kan'ani ameandika hayo leo Ijumaa kwenye mtandao wa kijamii wa X na kuongeza kuwa, hatua ya kilaghai na ya majivuno ya Marekani ya kujifanya inaguswa sana na masaibu ya watu wa Ghaza haipunguzi chochote katika jinai inazofanya Marekani dhidi ya Wapalestina. 

Amesema, Marekani ni muungaji mkono mkuu wa jinai za utawala wa Kizayuni hivyo kujifanya kuwa inasaidia kupelekewa chakula Wapalestina hakuwezi kuwasahaulisha walimwengu uungaji mkono wa pande zote wa Washington kwa ukatili na jinai za kivita zinazofanywa na Israel huko Ghaza.Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, viongozi wa Marekani wanafanya ulaghai wanapochochea mabanda yao ya propaganda yaeneze uongo kuhusu haki za binadamu nchini Iran na kamwe hawatoweza kusafisha sifa yao mbaya ya kushiriki katika jinai ya mauaji ya umati dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina huko Ghaza na Ukingo wa Magahiribi. Amesisitiza kuwa, hatua ya Marekani ya kutumia vibaya suala la haki za binadamu ni sehemu kuu ya siasa za mambo ya nje za Washington. Moja ya vielelezo vya mauaji ya kizazi yanayofanywa na Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ni kuuzingira kikamilifu ukanda huo na kuzuia kuingia na kutoka chochote hata wagonjwa na chakula na madawa. Utawala wa Kizayuni unafanya jinai na mauaji hayo ya kizazi kwa msaada na uungaji mkono kamili wa madola ya kiistikbari yakiongozwa na Marekani.

342/