Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Machi 2024

20:10:17
1445186

Al Atifi: Yemen kuainisha sheria mpya za vita mkabala wa Marekani na Uingereza

Mohamed al Atifi Waziri wa Ulinzi wa Yemen amesema kuwa Sana'a itaainisha sheria mpya za vita mkabala wa mashambulizi ya Marekani na Uingereza katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Televisheni ya al Masirah imeripoti kuwa, Waziri wa Ulinzi wa Yemen ametilia mkazo haja ya kuendelezwa oparesheni za kijeshi za vikosi vya ulinzi vya Yemen dhidi ya meli zenye mfungamano na Marekani, Uingereza na utawala ghasibu wa Israel.  

Mohamed al-Atifi ameongeza kuwa, Yemen itatumia nguuvu zake kuweka kanuni mpya za vita, ambazo Marekani, Uingereza, Wazayuni, na wafuasi wao watalipa gharama kubwa.

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Waziri wa Ulinzi wa Yemen amebainisha kuwa wananchi wa Yemen si wachochezi wala wachokozi, lakini jinai za kikatili zinazofanywa na utawala wa Israel huko Gaza zimeyachochea mataifa yanayopenda uhuru duniani kama vile watu wa Yemen, ambao wametangaza msimamo wao dhidi ya wavamizi. 

Amesema Yemen itaendelea kuzuia meli zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kupitia Bahari Nyekundu na katika mlango bahari wa Babul- Mandab; na kwamba Sana'a haitasitisha oparesheni za kijeshi dhidi ya meli za Marekani na Uingereza hadi hapo vita na mzingiro dhidi ya Gaza vitakapositishwa.  

Juzi Ijumaa Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa jeshi la taifa la Yemen alisema kuwa jeshi la nchi hiyo limezishambulia meli za Marekani na Israel katika Bahari ya Hindi katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kujibu uvamizi wa Marekani na Uingereza dhidi ya nchi hiyo.

342/