Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Machi 2024

20:10:36
1445187

Mkuu wa WHO aiambia Israel: 'Kwa jina la ubinadamu' futeni mpango wa kuivamia kijeshi Rafah

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeutaka kwa msisitizo mkubwa utawala wa Kizayuni wa Israel uchukue uamuzi wa kufuta mpango wake wa kuuvamia na kuushambulia kijeshi kupitia ardhini mji wa Rafah ulioko kusini ya Ukanda wa Ghaza, unaohimili vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala huo.

Mji huo wa kusini ya Ghaza umekuwa mwenyeji wa kupokea na kutoa hifadhi kwa idadi kubwa ya Wapalestina karibu milioni 2.4 wakazi wa ukanda huo ambao wamekimbilia huko kutokana na janga la vita.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameandika kwenye mtandao wa X, akisema: "nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za mpango wa Israel kuendelea na shambulio la ardhini dhidi ya Rafah". Dkt. Adhanom Ghebreyesus ameongezea kwa kusema: "kuongezeka zaidi ghasia katika eneo hili lenye watu wengi kutasababisha vifo na mateso mengi zaidi. Kwa jina la ubinadamu, tunatoa wito kwa Israel kutosonga mbele na badala yake kuchukua hatua kwa ajili ya amani." Utawala katili wa Kizayuni ulianzisha vita tarehe 7 Oktoba, 2023 kujibu operesheni ya kulipiza kisasi iliyofanywa na harakati za Muqawama za Ghaza, na kupelekea mamia ya Wazayuni kuchukuliwa mateka. Wapalestina wapatao 31,553, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijanawadogo, wameuawa shahidi hadi sasa katika mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya Ghaza. Halikadhalika, Mkuu wa WHO ametoa maanani kile kinachoitwa mpango uliobuniwa na utawala wa Israel wa kuhamisha watu kabla ya kuivamia kijeshi Rafah. Amesema, watu milioni 1.2 huko Rafah hawana mahali popote salama pa kuhamia.