Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Machi 2024

20:12:19
1445191

AFP: Viongozi wa harakati za muqawama wamekutana kuratibu mashambulizi dhidi ya Israel

Harakati ya Muqawama za Hamas, Jihad Islami, Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina na harakati ya Ansarullah ya Yemen zimefanya mkutano kwa ajili ya kuratibu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuliunga mkono na kulitetea taifa linalodhulumiwa la Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, limefichua kuwa, mkutano huo "muhimu" ulifanyika wiki iliyopita kujadili "njia za kuratibu mapambano dhidi ya Israel.

AFP imesema: "Mkutano muhimu ulifanyika wiki iliyopita ambapo viongozi wakuu kutoka Hamas, Jihad Islami, Popular Front for the Liberation of Palestine na harakati ya Ansarullah ya Yemen walijadili taratibu za kuratibu harakati za makundi hayo kuhusu hatua za mapambano katika hatua inayofuata."

Katika kikao hicho, harakati ya Ansarullah ya Yemen imethibitisha uwezo wake wa kuendeleza operesheni zake katika Bahari Nyekundu kwa nguvu kama ilivyokuwa hapo awali, dhidi ya meli zinazopeleka bidhaa na misaada kwa adui Mzayuni na kusisitiza kuwa, mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza hayatakufua dafu katika kuizuia harakati hiyo kutekeleza ahadi yake ya kuwatetea ananchi wa Palestina na mapambano yao.

Mkutano huo pia ulijadili jukumu la nyongeza la Ansarullah na harakati za mapambano za Palestina, iwapo Israel itavamia eneo la Rafah.

Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) halikubainisha eneo la mkutano huo na majina ya viongozi wa makundi ya Muqawama ya Palestina na Ansarullah ya Yemen walioshiriki katika mkutano huo. 

Wananchi wa Yemen wametangaza uungaji mkono wao wa wazi kwa mapambano ya Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel tangu utawala huo ghasibu ulipoanzisha vita vikali dhidi ya watu wa Gaza, tarehe 7 Oktoba mwaka jana baada ya harakati za mapambano za Palestina kutekeleza operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

342/