Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Machi 2024

20:14:27
1445197

Vikwazo vya upande mmoja; ukiukaji wa haki za binadamu

Balozi na Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika makao ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya huko Geneva Uswisi amesema kuwa leo hii madhara ya vikwazo haramu vya upande mmoja yamedhihirika wazi mbele ya walimwenu ambapo vimefanya hali ya migogoro ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi sambamba na kuchochea ukiukwaji wa haki za kimsingi za binadamu.

Ali Bahreini balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika makao ya Ulaya ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi amesisitiza kutokuwa na taathira ufumbiaji macho vikwazo hivyo baadhi ya wakati kutokana na madai ya kuzingatia masuala ya kibinadamu na kusema hilo halipunguzi chochote katika uharamu wa vikwazo hivyo."  Ali Bahreini amebainisha hayo katika mkutano uliofanyika mjini humo chini ya anwani "Taathira za hatua za upande mmoja kwa juhudi za kutuma misaada ya kibinadamu na utendaji wa pande husika katika masuala ya kibinadamu." Katika kipindi cha miongo 6 iliyopita, madola ya Magharibi na taasisi za kimataifa zimezidisha pakubwa utumiaji vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi nyingine. 

Mwanzoni mwa muongo wa sitini, ni chini ya asilimia 4 tu ya nchi ndizo ziliwekewa vikwazo na Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa. Lakini hivi sasa kiwango hicho kimeongezeka hadi asilimia 27. Kwa kuzingatia takwimu hizi, inaweza kudaiwa kuwa zaidi ya robo ya nchi na karibu theluthi moja ya uchumi wa dunia vinakabiliwa na vikwazo vya nchi za Magharibi au Umoja wa Mataifa. 

Ni wazi kuwa vikwazo hivi tajwa vinavyojumuisha vikwazo vya kiuchumi vinatumiwa na madola yenye  nguvu duniani kama wenzo muhimu wa kuzishinikiza nchi nyingine kimataifa. Vikwazo hivi vingi vinatekelezwa kwa visingizio mbalimbali kama kupiga marufuku uenezaji wa silaha za nyuklia au kuimarisha haki za binadamu lakini siku zote kuna malengo ya kisiasa na kababe nyuma ya vikwazo hivyo. 

Vikwazo vya upande mmoja licha ya kuwa na taathira hasi katika maisha ya watu katika jamii;  huathiri pia haki za mtu binafsi na jamii inayomzunguka kwa ujumla na hivyo kusababisha kukiukwa haki za binadamu. Utafiti wa matokeo ya vikwazo hivyo katika nchi zinazolengwa unaonyesha kuwa raia wa kawaida ndio waathirika wakuu wa mateso na taathira kuu za vikwazo vya nchi za Magharibi huku viwango vya haki za binadamu vikiukwa pakubwa kutokana na vikwazo hivyo. Utafiti uliofanywa na watafiti wa masuala ya kiuchumi, Matthias Neuenkirch na Florian Neumeier kuhusu athari za vikwazo kwa nchi mbalimbali unaonyesha kuwa vikwazo vinasababisha kukosekana usawa wa kipato, umaskini na kupungua ukuaji wa Pato la Taifa la nchi zinazolengwa. Kwa mfano  vikwazo vilivyowekwa na Marekani kati ya mwaka 1991 hadi 2018 vilizidisha kiwango cha umaskini kwa nchi zilizoathiriwa na vikwazo kwa karibu asilimia 3.5; na wakati huo huo vilipunguza kwa zaidi ya asilimia mbili kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kwa mwaka kwa nchi hizo.   

Utafiti kuhusu athari za vikwazo katika nchi kama vile Iraq na Haiti unaonyesha kuwa vikwazo hivyo vimesababisha ongezeko kubwa la vifo vya watoto, kuenea umaskini, uhamiaji, ukosefu wa chakula na dawa na matatizo mengine ya kijamii na kiuchumi.

Ingawa haki ya kupata chakula, makazi, huduma za afya na usalama wa kijamii ni moja ya mada muhimu zaidi za haki za binadamu na imejumuishwa katika Hati ya Kimataifa ya Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, hata hivyo vikwazo vya upande mmoja dhidi ya jamii nyingine vinatishia maisha ya watu, ustawi, huduma za afya na usalama wa chakula na kukiuka haki za binadamu. 

Kwa hiyo, ijapokuwa inadaiwa kuwa vikwazo hivi vimekusudiwa kwa serikali na mifumo ya kisiasa, lakini kivitendo raia wa kawaida wa jamii zinazolengwa ndio huathirika na kupata hasara kubwa kutokana na vikwazo hivyo vya upande mmoja. Alena Douhan, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa amesema kuhusu athari hasi za hatua za  upande mmoja kuhusu haki za binadamu kwamba: 'Utekelezaji wa vikwazo vya upande mmoja unaweza kusababisha ukiukwaji wa sheria za msingi za haki za binadamu.'