Main Title

source : Parstoday
Jumapili

17 Machi 2024

20:15:30
1445199

Waangalizi wa uchaguzi wa OIC: Russia imeandaa fursa za kupiga kura kwa makundi yote ya raia

Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kisiasa katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amesema kuwa Russia imeandaa fursa nzuri kwa raia kwa ajili ya kupiga kura.

Mohamed Salah Tekaya ambaye ni mwenyekiti wa kundi la waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuiya ya OIC katika uchaguzi wa rais wa Russia, amesema kuwa kusimamia uchaguzi ni moja ya kazi kuu ya kundi hilo na ni msingi wa “utawala wa sheria na uwazi katika uendeshaji wa uchaguzi". 

Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kisiasa katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ameishukuru Russia kwa kuwaalika kufuatilia zoezi la uchaguzi wa rais na kusema, wamebaini kuwa uchaguzi wa rais wa Russia una umuhimu mkubwa katika uhai wa nchi hiyo hususan katika maisha ya watu wa Russia. Tekaya amesema, ujumbe wa OIC umetembelea vituo vingi vya kupigia kura mjini Moscow na kushuhudia mchakato wa upigaji kura. "Tumeridhishwa kwamba Russia imewapatia fursa za kutosha watu wa nchi hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi", amesema Tekaya. 

Wakati huo huo Shakir Mohamoud Bandar Mkuu wa kundi la kufuatilia uchaguzi ndani ya jumuiya ya OIC ameeleza kuwa hii ni mara ya pili kwa jumuiya hiyo kufuatilia uchaguzi wa rais wa Russia. Ameongeza kuwa, OIC inaunga mkono uhusiano mzuri kati yake na Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Umoja wa Ulaya  na Umoja wa Afrika.Vladimir Putin (rais wa sasa), Nikolai Kharitonov wa Chama cha Kikomunisti, Vladislav Davankov wa Chama Kipya cha Wananchi na Leonid Slutsky kutoka Chama cha Demokrasia ya Kiliberali ndio waliochuana katika uchaguzi wa rais wa juzi nchini Russia. 

342/