Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:31:32
1445546

Yemen: Oparesheni dhidi ya meli za Israel zitaendelea

Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen imesisitiza leo katika radiamali yake kwa taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu oparesheni za kijeshi za vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo katika Bahari Nyekundu kuwa oparesheni hizo zitaendelea dhidi ya utawala wa Kizayuni hadi hapo utawala huo utakapositisha jinai zake katika Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen imesema imeshangazwa na hatua ya Baraza la Usalama la UN ya kulaani oparesheni za vikosi vya ulinzi vya Yemen katika Bahari Nyekundu zinazotekelezwa kwa lengo la kuinga mkono Gaza.  

Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeongeza kuwa: Taarifa ya Baraza la Usalama la UN kuhusu oparesheni za jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu na ya Kiarabu inaonyesha namna taasisi hiyo inavyotii na kusalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani ili kuunga mkono jinai katili za utawala wa Israel huko Ukanda wa Gaza. 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeendelea kubainisha kuwa: Ni fedheha kuona kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa karibu siku 200 sasa limeshindwa kutoa taarifa ya kulaani mauaji ya kila uchao yanayofanywa na adui Israel dhidi ya watoto na wanawake wa Gaza. Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeeleza kuwa, Baraza la Usalama lilipaswa kuizuia Marekani kuupatia silaha utawala ghasibu wa Kizayuni; silaha ambazo zinatumika kutekeleza mauaji ya kimbari ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza.

342/