Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:32:31
1445548

Thomas Friedman: Netanyahu ndiye kiongozi mbaya zaidi katika historia ya Kiyahudi

Mwandishi na mwanahabari wa Marekani, Thomas Friedman, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ataingia katika historia kama kiongozi mbaya zaidi katika historia ya Kiyahudi.

Friedman amesema katika mahojiano na gazeti la Israel la Haaretz kwamba: "Wacha niseme ukweli, nadhani hii ndio serikali mbaya zaidi ambayo Israel imewahi kuona. Ninaamini kuwa Netanyahu ataingia katika historia ya kuwa kiongozi mbaya zaidi katika historia ya Wayahudi, na sio tu katika historia ya Israel."

Friedman, mwandishi wa gazeti la Marekani The New York Times, ameeleza kwamba vita vya Waisraeli dhidi ya Gaza ni Vita halisi vya Pili vya Dunia. Amesema: "Wakati vilipoibuka vita vya Ukraine nilisema, hivi kwa hakika ndivyo "Vita vya Kwanza vya Dunia" na tunavyoviita Vita vya Kwanza vya Dunia havikuwa vita vya dunia.Friedman ameeleza kuwa vita vya Ukraine ni Vita vya Kwanza vya Dunia kwa sababu watu wanaweza kuvifuatilia kwenye simu zao za kiganjani, na wanaweza kutoa maoni yao juu yake, na athari mbaya za sekta ya kilimo ilikuwa ya haraka, vimekuwa na athari kwa bei ya chakula, na vimekuwa vita halisi vya dunia. Thomas Friedman ameendelea kusema: "Ninadai kwamba vita vya Israel dhidi ya Gaza kwa hakika ni Vita vya Pili vya Dunia. Kila mtu duniani ana maoni yake kuhusu vita hivyo, anavifuatilia na anaathiriwa navyo."

342/