Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:33:19
1445549

UN yasema 'imeshtushwa' na mashambulizi mabaya ya anga dhidi ya Waislamu wa Rohingya

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Katibu Mkuu wa umoja huo, António Guterres, "amesikitishwa" na ripoti za mashambulizi ya anga yanayoendelea nchini Myanmar ambayo yameua zaidi ya raia 20 katika kitongoji cha Minbya katika Jimbo la Rakhine siku ya Jumatatu.

"Kupanuka kwa migogoro katika Jimbo la Rakhine (ambalo wengi wao ni Waislamu) kunasababisha watu kuhama makazi na kuzidisha mapungufu na ubaguzi uliokuwepo hapo awali," msemaji huyo alisema.

Amesema: “Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na ripoti za mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na jeshi la Myanmar, ikiwa ni pamoja na katika kitongoji cha Minbya ambayo yanaripotiwa kuua na kujeruhi raia wengi."

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema: "António Guterres anatoa wito kwa pande zote kuzuia uchochezi zaidi wa mivutano ya kikaumu." 

Shambulizi la anga la Jumatatu ya jana lilipiga kijiji chenye Waislamu wengi cha Thar Dar mwendo wa saa 1:45 asubuhi baada ya ndege ya kivita kudondosha mabomu na kuua wanaume 10, wanawake wanne na watoto 10.

Taarifa zinasema kuwa mwanazuoni wa dini ya Kiislamu, Mawlawi U Hasa Nali (60) pamoja na mkewe na watoto watatu wameuawa katika tukio hilo.

342/