Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:34:18
1445551

Iran yalaani shambulio katika hospitali ya Al Shifa Ukanda wa Gaza

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kitendo cha ukatili na kinyama cha utawala wa Kizayuni cha kuishambulia hospitali ya al Shifa huko Ukanda wa Gaza.

Utawala wa Kizayuni unaotekeleza mauaji ya kimbari umedhihirisha vyema unyama wake kwa kushambulia vituo vya tiba na miundomsingi ya afya.  Katika jinai yake ya karibuni dhidi ya taasisi za afya, utawala wa Kizayuni jana asubuhi uliishambulia hospitali ya al Shifa katika Ukanda wa Gaza; na mbali na kuwauwa shahidi raia kadhaa wa Kipalestina, umepelekea mamia ya wengine kuwa wakimbizi, huku ukiwazingira wagonjwa, waandishi wa habari, madaktari na wahudumu wa afya ndani ya hospitali hiyo.  Kuhusiana na suala hili, Nasser Kanani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani jinai za utawala wa Kizayuni Ukanda wa Gaza na kusema: Hii si mara ya kwanza dunia inashuhudia wazi ukweli huu mchungu ambapo utawala wa Kizayuni unakiuka pakubwa sheria na kanuni zote za kimataifa , unaishambulia hospitali, unauwa, unawapiga, kuwajeruhi au unawazingira wafanyakazi wa sekta ya tiba, wagonjwa na majeruhi wa vita; na hivyo kukiuka kanuni za wazi kabisa za ubinadamu na sheria za kimataifa kuhusu masuala ya kibinadamu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mara nyingine tena amekumbusha wajibu wa jamii ya kimataifa kuhusu hali chungu ya Ukanda wa Gaza, na kuutaka Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kutekeleza wajibu wao kimataifa ili kuzuia kuendelea jinai za kivita zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel. Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitangaza kuwa jumla ya watu elfu 32 wameuliwa shahidi hadi sasa tangu utawala wa Kizayuni uanzishe vita dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana. 

342/