Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:36:25
1445555

WHO: Oparesheni za kijeshi dhidi ya Rafah zitasababisha maafa halisi

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitahadharisha Israel kuhusu oparesheni yoyote ya kijeshi katika mji wa Rafah na kusema, misaada ambayo imewasili Ukanda wa Gaza haitoshi kukidhi mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.

Utawala wa Kizayuni unaotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina umeonyesha ukatili wake kwa kushambulia vituo vya matibabu na miundombinu ya afya. Katika jinai yake ya jana asubuhi utawala wa Kizayuni umeishambulia hospitali ya al Shifaa huko Ukanda wa Gaza na mbali ya kuwauwa shahidi raia kadhaa wa Kipalestina, umepelekea mamia ya wengine kuwa wakimbizi, huku ukiwazingira wagonjwa, waandishi wa habari, madaktari na wahudumu wa afya ndani ya hospitali hiyo.   

Msemaji wa WHO Dakta Margareth Harris amesisitiza kuwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika hospitali ya al Shifa huko Gaza hayawezi kuhalalisha kwa namna yoyote. Harris ameendelea kusisitiza kuwa pande zote zinapasa kuheshimu na haki za binadamu na kuruhusu hospitali katika Ukanda wa Gaza kuendelea kutoa huduma. Amesema Gaza iko kwenye ukingo wa njaa, na kwamba watoto kadhaa wamepoteza maisha kutokana na njaa. Msemaji wa Shirika la Afya Duniani bila ya kuashiria ukwamishaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni na hatua yake ya kuuzia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza amekiri kuwa misaada ambayo imeingia Ukanda wa Gaza hadi sasa haitosho kukidhi mahitaji ya wakazi wa eneo hilo. 

342/