Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:36:50
1445556

BBC kuchunguza matumizi ya mitandao ya kijamii ya wafanyakazi wake baada ya ripota 'kuunga mkono' ujumbe dhidi ya Israel

Shirika la Utangazaji la Serikali ya Uingereza, BBC litachunguza matumizi ya mitandao ya kijamii baada ya mwandishi wake "kuunga mkono" jumbe zinazoilaumu Israel kama utawala wa "mauaji ya kimbari" na kuunga mkono haki ya Wapalestina kupinga uvamizi wa Israel.

BBC imesema inashughulikia ukiukaji wa miongozo yake ya mitandao ya kijamii, ambayo inahitaji kutokuwa na msimamo wa upendeleo kabisa kutoka kwa wafanyikazi wake, kwa umakini mkubwa, na kwamba "itachunguza kila kesi kwa undani."

Hatua hiyo inakuja baada ya mwandishi Soha Ibrahim wa BBC ya Kiarabu ku "like" jumbe kadhaa kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani Twitter, ikiwa ni pamoja na ujumbe uliotolewa baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Oktoba 7 ambao uliwafananisha wanachama wa Harakati ya Mpambano ya Palestina, Hamas na "wapigania uhuru.”

Ripota huyo wa BBC pia aliunga mkono (like) video ambayo ilisema Israel ilikuwa inalenga kutekeleza "mauaji", pamoja na jumbe kadhaa zinazosema Israel ilikuwa ikitekeleza "mauaji ya kimbari".

Miongoni mwa jumbe zilizoungwa mkono na ripota huyo wa BBC ni ule wa kiongozi wa zamani wa chama cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn, akitetea maandamano  ya waungaji mkono wa Palestina yanayofanyika kote Uingereza, ambapo mwanasiasa huyo alisema, "maandamano ya kupinga mauaji makubwa ya raia sio tishio kwa demokrasia."

Mwanahabari huyo mwenye makazi yake London pia ameunga mkono ujumbe ambao ulimkosoa mwajiri wake mwenyewe, yaani shirika la BBC, kwa kutoangazia ipasavyo uvamizi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Mapema mwezi huu, Kituo cha Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari (CFMM) kilisema katika ripoti iliyopewa jina la "Media Bias Gaza 2023-24" kwamba vyombo vya habari vya Uingereza vimeshindwa kuakisi vita vya Gaza kwa njia ya haki.

342/