Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Machi 2024

14:37:21
1445557

Forensic Architecture yaishutumu Israel kwa "kufanya mauaji ya kimbari" huko Gaza

Shirika la Forensic Architecture limesema kuwa Israel inatekeleza "ugaidi wa kijiografia" ili kupanua operesheni ya kuwahamisha wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa mabavu, likibainisha kuwa hatua hizi zinaonyesha mwelekeo wa kufanya uhalifu wa mauaji ya kimbari.

Kwa mujibu wa shirika hilo, ambalo linajishughulisha na kutambua uhalifu wa kikatili unaofanywa na mataifa na makundi mbalimbali, kinachofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza kinawakilisha "mauaji ya kimbari".

Jeshi la utawala ghasibu wa Israel lilitoa maagizo ya kuwahamisha zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wakiishi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza katika siku moja, na kuwataka waende kwenye Bonde la Gaza (Wadi Gaza) kupitia Mtaa wa Salah al-Din, ambao lilisema ungekuwa njia salama.

Hata hivyo, shirika Forensic Architecture linasema kuwa mtaa huo ulikumbwa na mashambulizi mtawalia ya vikosi vya jeshi la Israel, ambayo yaliua makumi ya raia.

Limesema, Israel pia iliweka mitego yake katika mtaa wa Salah al-Din na kuanzisha vituo vya ukaguzi vya kijeshi, hasa katika eneo linalounganisha barabara hiyo na Wadi Gaza, na kutekeleza mauaji dhidi ya raia.

342/