Main Title

source : Parstoday
Jumatano

20 Machi 2024

13:31:47
1445747

Mshauri wa zamani wa White House ametaka Wapalestina wahamishwe Ghaza na kupelekwa jangwani

Mshauri wa zamani wa Ikulu ya Marekani (White House) Jared Kushner amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel inapasa uwaondoe Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na kuwahamishia kwenye jangwa la Negev kusini mwa ardhi zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Kwa mujibu wa gazeti la Guardian, Kushner, ambaye ni mkwe wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye Chuo Kikuu cha Harvard na kutamka bayana kwamba, kama angekuwa kiongozi wa Israel, "kipaumbele chake kikuu" kingekuwa ni kuwaondoa raia kutoka mji wa kusini wa Ghaza wa Rafah, na kwamba kwa kutumia "diplomasia" ingewezekana kirahisi kuwaingiza Misri. Amesisitiza kwa kusema: "lakini pamoja na hayo, ningekuweka sawa tu Negev nikajaribu kuwahamishia watu huko". Mshauri huyo wa zamani wa Ikulu ya Marekani amesisitiza kwa kusema: "nadhani hilo ndilo chaguo bora, na kwa njia hiyo kuweza kuingia (Ghaza) na kumaliza kazi".

Kwa mujibu wa Guardian, Kushner, ambaye yeye mwenyewe ni Myahudi amesifu kile alichokiita uwezo wa "thamani kubwa" wa "hali ya eneo la maji" wa Ghaza na kupendekeza kwamba Israel ingepasa iwaondoe raia wakati "inausafisha" Ukanda huo.

 "Ni hali ya kusikitisha kidogo huko, lakini katika jicho la mtazamo wa Israel, ningefanya kila niwezalo kuwahamisha watu na kisha kuisafisha," ameendelea kueleza mshauri huyo wa Trump. Katika mahojiano hayo, Kushner amemalizia kwa kudai kuwa, hadhani kama Israel imesema haitaki Wapalestina warudi tena baadaye katika eneo la Ukanda wa Ghaza.../


342/