Main Title

source : Parstoday
Jumatano

20 Machi 2024

13:34:40
1445752

UN yashtushwa na mashambulizi mabaya ya anga ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres "amesikitishwa" na ripoti za mashambulizi ya anga yanayoendelea nchini Myanmar ambayo yameua zaidi ya raia 20 katika kitongoji cha Minbya katika jimbo lenye Waislamu wengi la Rakhine siku ya Jumatatu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisem: "Kupanuka kwa migogoro katika Jimbo la Rakhine (ambalo wengi wao ni Waislamu) kunasababisha watu kuhama na kuzidisha udhaifu na ubaguzi uliokuwepo hapo awali."

Kumekuwa na makabiliano makali katika jimbo la Rakhine magharibi mwa Myanmar kufuatia kile kinachodaiwa na serikali kuwa eti ni "mashambulizi" dhidi ya vikosi vya usalama mnamo Novemba, ambayo yaliashiria mwisho wa usitishaji mapigano ambao ulizingatiwa zaidi tangu mapinduzi ya kijeshi mnamo 2021.

Msemaji huyo aliongeza kuwa Katibu Mkuu anatoa wito kwa pande zote kuzuia uchochezi zaidi wa mivutano ya jumuiya,"

Shambulio la anga la Jumatatu lilipiga kijiji chenye Waislamu wengi cha Thar Dar baada ya ndege ya kivita kudondosha mabomu na kuua wanaume 10, wanawake wanne na watoto 10.Jamii ya Warohingya yenye Waislamu wachache imekuwa ikikabiliwa na mateso nchini Myanmar yenye Mabudha wengi kwa miongo kadhaa. Takriban milioni moja kati yao wamekimbia makazi yao kufuatia mauaji ya halaiki yaliyoongozwa na jeshi mnamo 2017.

Takriban wakimbizi milioni wa Rohingya kwa sasa wanaishi katika kambi zilizojaa watu katika wilaya ya Cox's Bazar ya Bangladesh, ambayo inashiriki mpaka na Myanmar, wakati wengi wanaotafuta hifadhi wametawanyika katika nchi jirani kama India.

Viongozi wa kijeshi nchini Myanmar wanadai kuwa Waislamu wa jamii ya  Rohingya ni raia wa kigeni na wamekataa kuwapa uraia.


342/