Kwa mujibu wa Iran Press, Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo leo kwenye ujumbe kwa taifa alioutoa kwa njia ya televisheni na kusisitiza kuwa, mwaka huu wa 1403 Hijria Shamsia utakuwa wa ustawi zaidi wa kiuchumi na kupunguza kiwango cha mfumuko wa bei pamoja na kuongeza huduma kubwa zaidi kwa wananchi.
Raus Raisi amegusia pia njama za maadui za kujaribu kutoa pigo kwa Iran ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, mshikamano, umoja na ushirikiano wa wananchi na viongozi ndio ufunguo wa kushinda njama zote za maadui. Amesema, kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran kwenye nyuga za kila namna kunamvunja moyo na kumkatisha tamaa adui.
Vile vile amegusia matukio ya eneo hili hususan vita vya Ghaza kwenye ujumbe wake huo wa mwaka mpya wa Kiirani wa 1403 Hijria Shamsia na kusema kuwa, muqawama wa kupigiwa mfano wananchi wa Palestina umewalazimisha mabeberu waupe utawala katili wa Israel mabomu ya mabilioni ya dola ili waangamize watu milioni mbili wa Ghaza, lakini wameshindwa.
342/