Main Title

source : Parstoday
Jumatano

20 Machi 2024

13:36:06
1445755

Mwaka mpya wa Hijria Shamsia; Mwaka wa Mapinduzi ya Kiuchumi kwa Kushirikisha Wananchi

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe muhimu kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa 1403 Hijria Shamsia na ameuita mwaka huo kuwa ni wa mapinduzi ya kiuchumi kwa kushirikisha wananchi.

Katika sehemu moja ya ujumbe wake huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia masuala muhimu kwa Iran katika mwaka ulioisha wa 1402 Hijria Shamsa ambao umemalizika mapema leo asubuhi na kulitaja suala la vita vya Ghaza na mateso wanayopata wananchi wa Palestina kuwa ni miongoni masuala machungu sana ya kimataifa kwa Iran.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amegusia pia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni mwezi wa machipuo ya kiroho na kimaanawi ambao mwaka huu pia umekwenda sambamba na kuanza msimu wa machipuo na mwaka mpya wa Hijria Shamsia na kuhimiza kufanyika jitihada kubwa zaidi ya mwaka ulioisha wa 1402 Hijria Shamsia katika kuliletea maendeleo ya kila upande taifa. 

Kuhusu mwaka huu mpya ulionza saa chache zilizopita wa 1403 Hijria Shamsia, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, huu ni mwaka wa Mapinduzi ya Uzalishaji kwa Kushirikisha Wananchi na kusisitiza kuwa kila mmoja anapaswa aweke ahadi ya kutekeleza kikamilifu majukumu yake katika nyuga tofauti kwa ajili ya kutatua masuala ya wananchi hasa ya kiuchumi na amewaombea wote mwaka uliojaa baraka, amani na mafanikio.

342/