Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

21 Machi 2024

13:29:49
1445933

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yafunguliwa Tehran

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yamefunguliwa katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Hijria Shamsia.

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa jioni ya jana (Jumatano) na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Mahdi Esmaili chini ya kauli mbiu "Nitakusoma".

Mashirika 160 ya uchapishaji yanaonyesha vitabu vyao vya Qur'ani na vya kidini katika eneo la Swala ya Ijumaa la Musalla Imam Khomeini katika kipindi chote cha maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran mwaka huu yana vitengo na sehemu 25, zinazojumuisha vitabu na programu, ufundi, sanaa za kidini, ushauri, vyuo vikuu, elimu na mafunzo, watoto, vijana, uvumbuzi na msingi wa maarifa, akili bandia, tafsiri ya Qur'ani, Nahj al-Balagha, Swala, Palestina na Kimbunga cha al Aqsa, familia na kuhifadhi Qur'ani kwa urahisi.

Kitengo cha mashirika ya uchapisha wa nakala za Qur'ani na vitabu vinavyohusiana na taaluma ya Qur'ani katika maonyesho ya mwaka huu ya Tehran kina taasisi 45 za Qur'ani na taasisi 24 za serikali.

Sehemu ya kimataifa ya maonyesho ya Qur'ani Tukufu ya Tehran inajumuisha  wawakilishi kutoka nchi 25 kama Uturuki, Algeria, Senegal, Russia, India, Ufaransa, Afrika Kusini, China, Canada n.k.

342/