Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

21 Machi 2024

13:30:22
1445934

Gazeti la Kirusi: Mhimili wa Moscow-Tehran-Beijing unaundika katika maji ya bahari

Gazeti la Russia la "Nezavisimaya Gazeta" limeandika kwamba muungano mpya unaundwa kaskazini mwa Bahari ya Hindi kati ya China, Russia na Iran, na kwamba mazoezi ya pamoja ya majini kati ya meli za kivita za nchi hizo tatu yanafanyika katika "Ghuba ya Oman" chini ya jina "Ukanda wa Usalama wa Baharini."

Gazeti hilo limeeleza katika ripoti yake kwamba mazoezi kama huyo yamekuwa yakifanyika tangu 2018, lakini mazoezi ya sasa yana umuhimu wa kipekee kwa Moscow kwa kuzingatia mzozo wa Ukraine.

Limesema uhusiano wa Russia na Iran pia unaimarishwa zaidi kutokana na kuanzishwa njia ya usafirishaji ya kaskazini-kusini.

Maneva hayo ya kijeshi ya baharini yaliyopewa jina la "Ukanda wa Usalama wa Baharini 2024" chini ya kauli mbiu "Pamoja kwa ajili ya Kudumisha Amani na Usalama" yalivishiriikisha vikosi vya majini vya Iran, Russia na China katika eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba elfu 17 kaskazini mwa Bahari ya Hindi.  jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo iliyokuwa nchi mwenyeji. 

Msemaji wa maneva hayo Admeri Tajuddini alisema kuwa mazoezi hayo ya baharini yamefanyika kwa lengo la kudhamini usalama wa njia za mawasiliano na kupambana na tatizo la uharamia na ugaidi wa baharini. Amesema, 'hivi sasa nchi 3 kuu yaani Iran, China na Russia; na nchi tano waangalizi ambazo ni Oman, Afrika Kusini, Pakistan, Kazakhstan na Jamhuri ya Azarbaijan zimeshirikishwa katika maneva hayo.'

342/