Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

21 Machi 2024

13:30:59
1445935

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Njia ya kukomesha dhulma kubwa ya kuwepo utawala wa Kizayuni itaendelea

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Njia ya kukomesha dhulma kubwa ya kuwepo utawala wa Kizayuni wa Israel itaendelea.

Ayatullah Khamenei amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya wananchi akizungumzia kuzama kwa utawala wa Kizayuni katika kinamasi cha Gaza na kuongezeka chuki za mataifa mbalimbali dhidi ya Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa jinai zinazofanywa na Israel. Amesema: Kadhia ya Gaza na mauaji ya zaidi ya watu elfu 30,000, wanawake, watoto, wazee na vijana, mbele ya macho ya ulimwengu eti uliostaarabika na unaodai kutetea haki za binadamu, ni kielelezo cha dhulma na giza linalotawala nchi za Magharibi.  

Ameongeza kuwa: Wamarekani na Wazungu sio tu kwamba hawakuzuia jinai za utawala ghasibu, bali tangu siku za mwanzo kabisa walitangaza uungaji mkono wao kwa kufanya safari katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kuupa utawala haramu wa Israel kila aina ya silaha kwa lengo la kuendeleza jinai za utawala huo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja kuonyeshwa uwezo wa Muqawama kuwa ni matunda mengine ya vita vya sasa vya Gaza na kusema: Uwezo na nguvu ya Muqawama vimevuruga mahesabu ya Wamarekani na kuonyesha kwamba, Wamarekani sio tu kwamba hawawezi kutawala eneo hili la Magharibi mwa Asia, lakini pia hawawezi hata kuendelea kuwepo katika eneo hilo na wanalazimika kufunga virago na kuondoka.Vilevile amekutaja kudhihirika wazi hali mbaya na mgogoro unaousumbua utawala wa Kizayuni wa Israel mbele ya macho ya walimwengu wote kuwa ni ukweli mwingine wa matukio ya Gaza. Amesema: Kwa kuingia katika vita vya Gaza, utawala wa Kizayuni umetumbukia kwenye kinamasi na kushindwa, bila ya kijali kama utaondoka au kubakia katika eneo hilo. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa Marekani imechagua nafasi mbaya zaidi katika kadhia ya Gaza na kusema: Maandamano ya wananchi ya kuitetea Palestina katika mitaa ya London, Paris na Marekani kwenyewe, kwa hakika ni tangazo la chuki dhidi ya Marekani. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mahesabu potofu ya Marekani katika kadhia ya Gaza yameifanya nchi hiyo ichukiwe kote duniani na kuongezeka chuki dhidi yake mara kumi katika eneo la Asia Magharibi. Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono na kupongeza Muqawama na inausaidia kadiri inavyowezekana. Amesema: Inapaswa kueleweka kuwa, kwa hakika makundi ya Muqawama na mapambano ndiyo yanafanya maamuzi na kuchukua hatua, na yako katika njia ya haki.

342/