Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

21 Machi 2024

13:32:31
1445938

Sunak abanwa koo baada ya mpango wa kuwapeleka wakimbizi Rwanda kusitishwa

Mpango wa Serikali ya Uingereza, wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda, umepata pigo jingine baada ya Bunge la Wawakilishi kupiga kura ya kurejesha mapendekezo yao ya awali, ambayo yalikataliwa na Bunge.

Wachambuzi wa mambo wanasema uamuzi wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza dhidi ya mpango wa serikali ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, unaonesha mgawanyiko mkubwa kuhusu muswada wa usalama wa nchi ya Rwanda, ambao waziri mkuu Rishi Sunak na serikali yake wamekuwa wakiupigia debe.

Mpango huo wa serikali ya Uingereza umekuwa ukipingwa vikali na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, yanaosema Rwanda haiwezi kuwa nchi salama kwa wakimbizi na wahamiaji hao.

Mapema mwaka huu Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya (ECHR) ilipasisha dikrii nambari 39, ambayo ilisimamisha kwa dharura na kwa muda mpango wa kuwapeleka Rwanda wahamiaji na waomba hifadhi walioko Uingereza.

London imekuwa ikisisitiza kuwa, itaingia makubaliano mapya na Kigali kwa ajili ya kufufua mpango wake huo wa kuhamishia waomba hifadhi Rwanda, licha ya hukumu ya Mahakama ya Juu ya Uingereza kusema mpango huo ni kinyume cha sheria.

Sunak amekuwa akipigia debe mpango huo akidai kuwa, watu wa Uingereza ndio wanaopaswa kuamua ni nani atakayeingia nchini humo na si magenge ya uhalifu au mahakama za nchi za kigeni.

Mahakama ya Juu ya Uingereza ilisema mwaka uliopita kwamba, mpango wa serikali ya London wa kuwapeleka nchini Rwanda wakimbizi na waomba hifadhi walioko nchini humo unakiuka sheria. Ilisema mpango huo unawaweka katika hali hatarishi wakimbizi hao, hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi yao waliikimbia nchi yao ya Rwanda na kuwarejesha huko ni kutawaweka hatarini.

342/