Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

22 Machi 2024

14:22:06
1446120

Hujjatul-Islam Ali Akbari: Maadui wasubiri operesheni zijazo za Kimbunga cha al-Aqsa

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema maadui wa Palestina wanapasa kusubiri operesheni ya pili, ya tatu na hata ya nne ya Kimbunga cha al-Aqsa kutoka kwa makundi ya muqawama.

Katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya Tehran, Hujjatul-Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari ameashiria jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, matokeo ya Kimbunga cha al-Aqsa ni dhihirisho la kusimama kidete muqawama na kutengwa Israel.

Amesema operesheni mfano wa Kimbunga cha al-Aqsa dhidi ya Israel zitaendelea kushuhudiwa hadi pale utawala wa Kizayuni utapofutwa katika ramani yenye kupendeza ya Palestina.

Tarehe 7 Oktoba, 2023, wanajihadi wa Palestina walianzisha Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ili kukabiliana na jinai na ukatili wa Israel. Operesheni hiyo ilikuwa ya kipekee kwa ukubwa wake wa kijiografia na uwepo mpana wa makundi ya wapiganaji wa Kipalestina.Hujjatul-Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari amebainisha kuwa, maadui wa Palestina wanapasa kusubiri operesheni nyingine kadhaa zinazoshabihiana na Kimbunga cha al-Aqsa kutoka makundi ya muqawama katika eneo. Katika sehemu nyingine ya hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Hujjatul-Islam Haj Ali Akbari ameyataka mataifa ya Kiislamu kujiandaa na kushiriki kwa wingi katika maadhimisho na maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds. Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema siku hii ambayo huadhimishwa kote duniani katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, inapasa kuwa zilzala ya kisiasa dhidi ya utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake.

342/