Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

22 Machi 2024

14:25:23
1446125

Guterres aonya dhidi ya "sera za kindumakuwili" kuhusu mafaili ya Ukraine na Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameionya jamii ya kimataifa dhidi ya "sera za kindumakuwili" katika kushughulikia mafaili ya Ukraine na Gaza.

Guterres alitoa onyo hilo jana katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel, baada ya mkutano wa baraza hilo mjini Brussels.

Guterres amekosoa "hali ya mchafukoge inayoshuhudiwa duniani, na vilevile ukwepaji wa adhabu, ambapo serikali au makundi yenye silaha yanaamini kwamba yanaweza kufanya chochote kutokana na ukosefu wa uwajibishwaji."

António Guterres amesisitiza umuhimu wa kuzingatia "Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa, usalama wa nchi mbalimbali, na sheria za kimataifa za kibinadamu."Pia ameleza masikitiko yake kutokana na "idadi isiyo na kifani ya raia waliouawa huko Gaza" katika kipindi chake kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Guterres amesema kuwa "msingi mkuu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu ni kulinda raia." Amesisitiza kuwa "kuna ulazima wa kuheshimu kanuni huko Ukraine kama ilivyo huko Gaza, bila ya kutumia sera za kindumakuwili."

342/