Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

23 Machi 2024

14:32:13
1446300

The Washington Post: Kauli za Kushner kuhusu Gaza ni dalili ya sera ya baadaye ya Trump

Gazeti la Marekani la The Washington Post limeripoti kuwa muhula wa pili wa Donald Trump, iwapo atashinda uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani, "huenda ukamaanisha uungaji mkono mkubwa zaidi wa Washington kwa watawala wa sasa wa Israel wanaotaka kuwafukuza Wapalestina kutoka Gaza na kulikalia tena kwa mabavu eneo hilo."

The Washington Post iliripoti jana Ijumaa kwamba wakati ulimwengu unafikiria jinsi sera ya kigeni ya utawala wa pili wa Donald Trump inaweza kuonekana, matamshi ya washauri na watu wa familia yake yanatoa ushahidi muhimu kuhusu sura itakavyokuwa.

Gazeti hilo limesema, kauli za hivi karibuni za Jared Kushner kuhusu mzozo kati ya Israel na Gaza zimezua mijadala mingi, kwa sababu Trump, kupitia Kushner, aliyekuwa mshauri wake katika masuala ya Mashariki ya Kati, ametuma ishara kwamba kipindi cha pili cha utawala wa wake kitakuwa na maana ya himaya na uungaji mkono mkubwa zaidi wa Marekani kwa Waisraeli wanaotaka kuwafukuza Wapalestina kutoka Gaza na kulikalia tena kwa mabavu eneo hilo."

Washington Post imeripoti kuwa, wazo kwamba "mipaka ya Gaza inaweza kubadilishwa, na kwamba Wapalestina wa eneo hilo hawawezi kurejea makwao, linakinzana moja kwa moja na sera ya sasa ya Marekani, ambayo inasisitiza juu ya haki ya watu wa Gaza kubaki Gaza katika mipaka yake ya sasa.

Gazeti hilo limeandika kwamba, “kuna mantiki inayokubalika katika msimamo huu, kwa kuwa vitendo vya kuhamisha watu kwa lazima vinaweza kuwa "ushahidi wa mauaji ya kimbari,” kama ilivyowasilishwa katika kesi ya Afrika Kusini kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki.Kushner ambaye pia ni mkwe wa Donald Trump ametoa wito kwa "Israel" kutekeleza mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza na kuwapeleka katika Jangwa la Negev, ili kutumia eneo la ufukwe la Ukanda wa Gaza. Jared Kushner aliongeza kuwa, kama angekuwa afisa katika serikali ya Israel, kipaumbele chake cha kwanza kingekuwa kuwaondoa Wapalestina kutoka Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na "kwamba kupitia diplomasia itawezekana kuwahamishia Misri."

342/