Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

23 Machi 2024

14:35:14
1446305

Majeshi ya India, Msumbiji, Tanzania katika mazoezi ya pamoja Bahari ya Hindi

Mazoezi ya pamoja kati ya majeshi ya majini ya Msumbiji, Tanzania na India yalianza Alhamisi katika pwani ya Afrika Mashariki katika Bahari ya Hindi.

Katika taarifa yake, Jeshi la Wanamaji la India lilisema zoezi hilo lililoanza Machi 21 litaendelea hadi tarehe 29 mwezi huu na litagawanywa katika awamu mbili.

Katika awamu ya kwanza, kuanzia Machi 21 hadi 24, meli za kivita za India za Tir na Sujata zitaungana na wanamaji wa Tanzania na Msumbiji katika bandari za Zanzibar na Maputo.

Taarifa imesema: "Awamu hii itajumuisha shughuli kama vile kuzima moto, kukamata meli, matibabu, uokoaji wa majeruhi na operesheni za kupiga mbizi.

Awamu ya pili, kuanzia Machi 24 hadi 27, itajumuisha kukabiliana na vitisho visivyo vya kawaida, kufanya mazoezi ya kutafuta na kukamata, ustadi wa kuendesha mashua na mazoezi ufyatuaji mizinga. Aidha kutakuwa na mazoezi ya kulinda doria.

Zoezi la kwanza la pande tatu mnamo Oktoba 2022 lilihusisha meli ya kivita ya India INS Tarkash na wanamaji wa Tanzania na Msumbiji.

342/