Main Title

source : Parstoday
Jumapili

24 Machi 2024

14:19:12
1446521

Jeshi la Anga la Syria latungua makombora ya Israel karibu na Damascus

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria vimefanikiwa kutungua makombora mengi yaliyovurumishwa na jeshi la Israel karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Syria, mapema Jumapili, ndege za kijeshi za Israel "zilifanya mashambulizi ya anga kutoka upande wa Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu, na kulenga maeneo kadhaa karibu na Damascus."

Ripoti hizo zimeongeza kuwa vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria vilitungua aghalabu ya makombora hayo. Hakukuwa na majeraha katika hujuma hiyo, lakini kulikuwa na hasara katika majengo.

Utawala haramu wa Israel mara nyingi hufanya mashambulizi ya anga kwenye vituo vya kijeshi nchini Syria, hasa vile vya kundi la Hizbullah ya Lebanon.

Hizbullah imekuwa na mchango mkubwa katika kulisaidia jeshi la Syria katika vita vyake dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na madola ya kigeni hasa utawala wa Kizayuni wa Isarel

Tangu kuanza mashambulizi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni nchini Syria mwaka 2011, Israel imejitokeza kama muungaji mkono mkubwa wa makundi ya kigaidi ambayo yanapinga uongozi uliochaguliwa kidemokrasia wa Rais Bashar al-Assad.

Mashambulizi ya hivi karibuni pia yanakuja huku kukiwa na ongezeko la vitendo vya uchokozi vya Israel dhidi ya Syria. Siku ya Jumanne, utawala wa Israel pia ulishambulia maeneo kadhaa ya kijeshi ya Syria karibu na Damascus.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria inasema Israel inajaribu sana kuficha kushindwa kwake katika Ukanda wa Gaza kwa kushambulia ardhi ya Syria.