Main Title

source : Parstoday
Jumapili

24 Machi 2024

14:23:58
1446530

Wasiwasi wa Marekani kuhusu muungano wa Iran, Russia na China

Kamanda wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) Jenerali Michael E. Kurilla amebainisha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa ushirikiano kati ya Iran, China na Russia na kudai kuwa ushirikiano wa nchi hizo utakuwa na"matokeo mabaya ya kimataifa".

Amesema hayo katika kikao cha Kamati ya Majeshi ya Baraza la Wawakilishi la Marekani alisema Iran, Russia na China zinazidi kuimarisha uhusiano wao.

Alidai kuwa "kwa pamoja, Iran, Russia, na China zinaimarisha uhusiano wao na kuendeleza mazingira yenye kuibua machafuko kwa maslahi yao. Vile vile amezungumzia uwezo wa Iran wa kuzalisha ndege zisizo na rubani na kusafirisha mafuta ghafi licha ya vikwazo vya Marekani. "Tunachokiona ni Iran kuitegemea China na Russia nayo inaitegemea Iran." Aidha amesema Iran inaiuzia China asilimia 90% ya mafuta yake yote yaliyowekewa vikwazo na Marekani.

Katika miaka ya hivi karibuni, kufuatia kuimarishwa uhusiano wa karibu wa Iran na Russia na China, na pia kupanuka kwa ushirikiano kati ya nchi hizo tatu katika mashirika ya kieneo kama vile Shirika la Ushirikiano la Shanghai na BRICS, watawala wa Marekani wameeleza wasiwasi wao kuhusu uhusiano huo na kuuona kuwa ni tishio kwa maslahi yao.

Ukweli ni kwamba siasa na mienendo ya kibeberu ya Wamagharibi hasa Marekani katika uga wa kimataifa hususan katika eneo la Magharibi mwa Asia na vilevile siasa za uadui za Washington dhidi ya nchi huru au zisizofungamana na upande wowote kama vile Iran na Russia ni nukta ambayo imepelekea kuimarike jitihada za kuunda kambi kinzani ya kimataifa yenye kufadhilisha maamuzi yanayochukuliwa na nchi kadhaa. Hivyo kuwepo kambi hii inayopinga ubebebru kumepelekea kudidimia zaidi ushawishi wa Marekani duniaini.Mwaka 2018, baada ya Marekani kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA, vikwazo dhidi ya Iran viliwekwa tena, na tangu wakati huo vikwazo hivyo vimekuwa vikiongezwa nguvu kwa visingizio mbalimbali. Russia nayo iliwekewa vikwazo vya nchi za magharibi mwaka 2022 baada ya kuanza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine. China pia inakabiliwa na vikwazo kutoka kwa Marekani katika masuala ya biashara. Katika hali hiyo, Iran, Russia na China zimepanua uhusiano wao wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama na kusisitiza haja ya kuwepo mfumo wa pande nyingi duniani ili kuzuia ubabe na ubeberu wa Marekani. Hivi sasa nchi hizi tatu zimetiliana saini mapatano ya ushirikiano yenye thamamani ya mamia ya mabilioni ya dola. Kutokana na ushirikiano huo, Marekani imeingiwa na wasiwasi mkubwa. Kwa hakika, Marekani iko katika hali maalum, ambayo inashuhudia kupungua kwa ushawishi wake katika matukio ya kimataifa na katika upande wa pili dunia inashuhudia kuongezeka nguvu na ushawishi chanya wa Iran, Russia na China. Ushawishi wa nchi hizo tatu unaongezeka sambamba na kuundwa makundi mapya ya kiuchumi duniani ambayo yanaashiria kudhoofika madola ya Magharibi na kupata nguvu mpya madola ya mashariki.

342/