Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:19:05
1446745

Al-Azhar: Hatua za kimataifa mkabala wa jinai za Israel Ukanda wa Gaza zinakatisha tamaa

Imamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri amesema kuwa radiamali za jamii ya kimataifa mkabala wa vita vya Israel dhidi ya Gaza zinakatisha tamaa.

Sheikh Ahmed al Tayyeb ameeleza haya wakati akimlaki Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Cairo Misri. Viongozi hao wawili wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya mambo ya Ukanda wa Gaza. 

Sheikh al Tayyeb amesema, "Kile kinajiri sasa Ukanda wa Gaza kinatishia kudhoofisha juhudi za mawasiliano na maelewano ambazo tumekuwa tukizitekeleza kwa miaka mingi na kujaribu kuziba pengo kati ya Mashariki na Magharibi." Ameongeza kuwa hatua na radiamali za jamii ya kimataifa kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza ni za kukatisha tamaa na kuhuzunisha 

Imamu Mkuu wa Al Azhar aidha amepongeza misimamo ya watu kuwaungamkono raia wa Ukanda wa Gaza iliyodhihirishwa katika nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na chi za Magharibi na huko Marekani na kusema hata  baadhi ya Wayahudi wenye nia njema wamejitokeza hadharani wakitaka kusitishwa mashambulizi dhidi ya Gaza.

Katika mazungumzo hayo huko Cairo Misri, Karibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema: 'Natoa shukrani zetu kwa Al-Azhar kama sauti madhubuti inayotetea na kuunga mkono watu wa Palestina. Guterres, jana alitembelea kivuko cha Rafah kwa lengo la kutuma ujumbe kwamba ipo haja ya kusitishwa vita na jamii ya kimataifa kutimiza wajibu wake kwa kuchukua maamuzi na si kutoa maneno matupu." 

342/