Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:19:30
1446746

Saraya Al-Quds yaangamiza Afisa mmoja na wanajeshi 3 wa Israel katika shambulizi la kuvizia huko Tulkarm

Brigedi za al Quds (Saraya al Quds) Batalioni ya Tulkarm imetangaza kuwa wanachama wake wamevamia gari lililokuwa na afisa mmoja na wanajeshi watatu wa Israel kaskazini mwa Tulkarm katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwaangamiza wote.

Haya yanajiri saa chache baada ya jeshi la Israel kutangaza habari ya kuuawa afisa wake na kikosi cha makomando na kujeruhiwa wengine kadhaa katika operesheni ya kuvizia huko Deir Bzei’, Ramallah.

Batalioni ya Tulkarm imesema katika taarifa yake kwamba wapiganaji wake walifanya shambulizi la kuvizia kwenye lango la Deir Al-Ghusun, kaskazini mwa mji wa Tulkarm, ambapo walifuatilia nyendo za jeshi vamizi la Israel; na baada tu ya kuwasili gari lililokuwa limebeba afisa na askari askari 3 wa utawala huo waliwafyatulia risasi moja kwa moja na kuwaangamiza. Wapigania ukombozi hao wa Palestina waliondoka salama eneo hilo.

Tangazo la operesheni ya Tulkarm linakuja saa chache baada ya jeshi la utawala ghasibu wa Israel kutangaza habari ya kuuawa afisa mmoja wa jeshi  na kujeruhiwa vibaya afisa mwingine na mwanajeshi kadhaa katika operesheni iliyotekelezwa na Mujahid Barakat Mansour katika kijiji cha Deir Bzei’ karibu na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi, siku ya Ijumaa, ambaye aliuawa shahidi baada ya mapambano makali na wanajeshi hao.

Mapigano hayo yaliendelea kwa saa kadhaa, huku jeshi la Israel likishindwa kumkamata Mansour isipokuwa kwa kumlenga kwa helikopta iliyomrushia kombora na kumuua shahidi.

342/