Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:20:33
1446748

Kufeli propaganda dhidi ya Hamas na kuongezeka umaarufu wa harakati hiyo huko Gaza

Licha ya kuenea propaganda sumu za vyombo vya habari vya Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu, lakini kura za uchunguzi wa maoni zinaonyesha kuwa wakazi wengi wa Ukanda wa Gaza wanaridhishwa na utendaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (Hamas).

Kituo cha Utafiti wa Kisiasa cha Palestina kimefanya uchunguzi wa maoni na kuripoti kwamba Wapalestina waliowengi wanaridhishwa na utendaji wa harakati ya Hamas kufutia uvamizi wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa utafiti huo, zaidi ya asimilia 70 ya wakaazi wa Ghaza wanaridhishwa na utendaji wa Hamas. Kufuatia operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo tarehe 7 Oktoba, ambayo ilipelekea utawala huo kushindwa vibaya zaidi katika historia yake yote ya uvamizi, utawala huo licha ya kutekeleza mauaji ya halaiki huko Gaza, unajaribu kuhalalisha mauaji hayo kwa kueneza propaganda chafu dhidi ya Hamas kuwa eti harakati hiyo ya muqawama ndio chanzo cha mgogoro wa Gaza.

Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya pia zinasaidia kueneza propaganda hizo dhidi ya Hamas. Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alidai Ijumaa katika kikao cha Baraza la Usalama kuwa mauaji ya kimbari huko Gaza ni matokeo ya mashambulizi na unyanyasaji wa kingono wa Hamas dhidi ya Israel. Lengo muhimu la propaganda hizo kubwa limekuwa ni kuidhalilisha harakati ya Hamas mbele ya watu wa Gaza na kuhalalisha mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni yenye lengo la kuliangamiza kundi hilo la mapambano ya ukombozi wa Palestina. Hata hivyo, kinyume na propaganda za utawala ghasibu wa Israel na baadhi ya tawala za Kiarabu na hata Mamlaka ya Ndani ya Palestina yenyewe eti kwamba matukio ya Gaza ni natija ya operesheni zilizofeli za wanamuqawama dhidi ya utawala haramu na katili wa Israel, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Kisiasa cha Palestina yanaonyesha kuongezeka umaarufu wa wanaharakati wa Hamas huko Gaza.

Swali muhimu ni kuwa, je, ni kwa nini propaganda kali dhidi ya Hamas zimeshindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa?  Na je, ni sababu zipi zimepelekea kuongezeka umaarufu wa Hamas huko Gaza? Sababu muhimu zaidi ni sera zenye mwelekeo wa kimantiki za harakati ya Hamas. Baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, Hamas si tu kwamba haikusalimu amri kwa mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni huko Gaza, bali hata katika mazungumzo ya pande kadhaa, imesimama imara kuhusu misimamo yake na kukataa kusalalimu amri mbele ya matakwa ya kidhalimu ya Tel Aviv. Hamas sambamba na kutoa kipigo kikali dhidi ya utawala haramu wa Israel, ilikataa kuwaachilia huru mateka wa Kizayuni wakati wa makubaliano ya kusimamisha vita kwa muda. Sera za  harakati ya Hamas ziliufanya utawala wa Kizayuni kupata pigo kubwa la kiintelijensia, kisiasa na vilevile kijeshi. Sera hizo za  Hamas zimefanikiwa katika hali ambayo Marekani na nchi za Ulaya zinaendelea kuunga mkono kikamilifu utawala haramu wa Israel.

Kwa miaka mingi, vyombo vya habari vya Kizayuni vimekuwa vikieneza prapaganda bandia kwamba jeshi la Kizayuni ndilo lenye nguvu zaidi  katika eneo la Asia Magharibi na la nne kwa nguvu za kijeshi  duniani, lakini leo hii duru za kisiasa na vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwemo vya Marekani na nchi waitifaki wa utawala huo na hata makamanda na maafisa waliostaafu  wa Kizayuni wanakiri kushindwa kwa jeshi la Israel katika medani ya vita na kundi dogo la Hamas. Umaarufu wa Harakati ya Hamas umeongezeka kutokana na sababu hizo na kwa kuzingatia pia ukweli kwamba mapatano ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Tel Aviv hayajakuwa na manufaa yoyote kwa Wapalestina.

342/