Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:22:36
1446750

Iran na Oman zasisitizia udharura wa kukomeshwa mara moja jinai za Israel Ghaza

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wamefanya mazungumzo ya simu na kutilia mkazo wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa za kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhlumu na wasio na ulinzi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.

Hussein Amir-Abdollahian amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Al Busaidi na kulaani vikali jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza hususan vitendo vya kinyama na visivyo na chembe ya ubinadamu vinavyofanywa na Wazayuni kwenye hospitali iliyozingirwa kila upande ya al Shifaa sambamba na kuua wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo bila ya huruma.

Mawaziri hao wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman amegusia pia uhusiano unaozidi kustawi baina ya nchi zao na wamehimiza kuchukuliwa hatua zaidi za kutanua na kustawisha zaidi na zaidi uhusiano wa kidugu uliopo baina ya pande hizi mbili. 

Hayo yamekuja huku wananchi wa Iran wakiwa wamefanya maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali za nchi ukiwemo mji mkuu Tehran, kutangaza mshikamano na wananchi madhulumu wa Palestina wanaoendelea kuuawa kikatili, sambamba na kulaani jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wananchi wa Iran ya Kiislamu usiku wa kuamkia leo Jumatatu wamefanya maandamano ya nchi nzima wakieleza masikitiko yao kwa jinai zinazoendelea kufanywa na Wazayuni huko Ghaza, sambamba na kutangaza hasira zao kutokana na uovu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

342/