Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:23:54
1446752

Mkutano wa Umoja wa Mabunge unaendelea Geneva kwa kuhudhuriwa na Iran

Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani, kama chombo kikubwa zaidi cha utungaji sheria chenye nchi wanachama zaidi ya 180, ukiwemo ujumbe kutoka Iran unafanyika mjini Geneva Uswisi kwa kauli mbiu ya "Diplomasia ya Bunge, Ujenzi wa Daraja la Amani na Maelewano".

Ujumbe wa wabunge kadhaa wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) unashiriki katika mkutano huo ambao ulianza tarehe 23 Machi na utaendelea hadi tarehe 28 mwezi huu.

Katika mkutano huo wa Geneva, ujumbe wa Iran unashiriki pia katika kamati za kitaalamu za pande nne zinazojumuisha vikao vya wabunge, semina za wabunge wanawake, vikao vya kujadili amani na usalama wa kimataifa, demokrasia, haki za binadamu, ustawi endelevu na masuala ya Umoja wa Mataifa.   

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, katika siku ya kwanza ya mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani huko Geneva mabunge ya nchi za Kiislamu na Baraza la Mabunge ya Asia yamefanya vikao mbalimbli baina yao; ambapo ujumbe wa Iran umesisitiza kuwa mabunge ya nchi za Kiislamu na Asia yanapasa kudhihirisha msimamo wa pamoja na kupinga jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.  Mwakilishi wa utawala wa Kizayuni hakuruhusiwa kutoa hotuba katika mkutano huo wa Umoja wa Mabunge Duniani; ambapo ukumbi wa mkutano uliingiwa na wasiwasi, huku washiriki wakipinga vikali mwaklishi wa bunge la Israel kuhutubia. Wawakilishi wa mkutano huo wametaka kusitishwa vita haraka iwezekanavyo huko Ukanda wa Gaza na kukomeshwa mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni. Umoja wa Mabunge Duniani ni taasisi ya kwanza ya bunge ambayo imeweza kupata nafasi kubwa katika uwanja wa mahusiano ya kimataifa katika mjadala wa diplomasia ya mabunge ya pande kadhaa.

342/