Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

25 Machi 2024

14:25:35
1446755

'Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kutangaza mshikamano na Wapalestina'

Mwanaharakati mmoja na mtafiti wa Chuo Kikuu raia wa Nigeria amewataka wananchi wa nchi za Afrika wajitokeze kwa wingi kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani akisisitiza kuwa hiyo ni siku ya kutangaza uungaji mkono kwa wananchi madhlumu wa Palestina wanaofanyiwa ukatili wa kutisha na Israel.

Muhammad Issa Ahmad amesema hayo kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Iran Press katika mji wa Zaria huko Kaduna Nigeria na sambamba na kugusia umuhimu mkubwa wa Siku ya Kimataifa ya Quds amesema kuwa, siku hiyo iliyotangazwa na Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muhimu sana na kuna haja kwa wananchi wote wa Afrika ambao wana uzoefu mchungu wa kukandamizwa na ukoloni wa madola ya Magharibi, wajitokeze kwa wingi zaidi mwaka huu kuadhimisha siku hiyo.

Vile vile amesema kuwa, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anaendeleza njia ile ile ya Imam Khomeini MA ya ukombozi wa Palestina na kusisitiza kuwa, Ayatullah Khamenei ana nafasi kubwa katika kuyabakisha hai malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina na leo hii tunaona mwito wake wa kuungwa mkono wananchi wa Ghaza ulivyopokewa vilivyo na kuitikiwa ipasavyo katika kila kona ya dunia.

Mwanaharakati huyo mkubwa na maarufu wa masuala ya haki za binadamu wa huko Zaria Nigeria pia amesema kuwa, siku itafika ambapo walimwengu watashuhudia wananchi wa Palestina wanaishi kwa usalama na amani bila ya kumwagwa damu zao, tofauti na hivi sasa ambapo Wazayuni hawajali hata kidogo kumwaga damu za Wapalestina wasio na hatia.

342/