Main Title

source : Parstoday
Jumatano

27 Machi 2024

13:37:10
1447192

Mateka wa Kipalestina waongezeka pakubwa katika jela za utawala wa Kizayuni

Klabu ya Mateka wa Palestina imetangaza kuwa kuna ongezeko kubwa sana la mateka wa Kipalestina wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni bila ya kuhukumiwa.

Klabu ya Mateka wa Palestina imetangaza kuwa tangu kuanza mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza Okktoba 7 mwaka jana hadi sasa idadi ya raia wa Palestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia watu 3,558. 

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, idadi ya mateka wa kike walioko katika magereza ya utawala wa Kizayuni bila ya kuhukumiwa pia imeongezeka zaidi ikilinganishwa na siku za nyuma na kufikia kesi 19. 

Utawala wa Kizayuni unawafungia jela Wapalestina bila ya kuwahukumu na bila ya kuwafungulia mashtaka. 

Utawala wa Kizayuni unatumia sera ya kuwatia mbaroni na kuwaweka kizuizini raia wa Palestina bila ya mashtaka mahususi na pasina kuwafikisha mahakamani, jambo linalowanyima raia hao haki ya kuwasiliana na mawakili wao ili kujua sababu za kukamatwa kwao. 


342/